MCH. MAMA MGETA: ULINDE MOYO WAKO

Siku ya Jumapili 27/09/2015, Mch. Mama Mgeta aliweza kuhubiri Habari Njema katika kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God kwa Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare juu ya  Kuulinda Moyo alikuwa na haya ya kuhubiri; Tutasoma kitabu cha Isaya 26:3, Biblia inasema “Nitamlinda Yule ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamiilifu kwa kuwa anautumaini.” Watu wa dunia wanaweza kuwa ana amani kwasababu wana biashara kubwa na inaenda vizuri, anacheo kizuria, ana akaunti na ina fedha nyingi, lakini nachotaka kusema ni kwamba, amani kwa watu wa Mungu inapatikana kwa Mungu, haijalishi unaishi nyumba ya nyasi, nyumba ya kupanga, hujavaa suti ila tambua kuwa amani ya Mungu inatawala kwenye moyo wa mwanamke au kwenye moyo mwanaume hapo ndipo amani ya kweli ilipo.
 
Mch. Mama Mgeta

Moyo wa mtu ukimtegemea Mungu, mtu huyu atakuwa hana majungu kanisani, hatatikiswa na jambo lolote, haijalishi unaishi maisha gani bali Mungu anakulinda. Ndugu zangu mtambue kuwa mnalindwa na nguvu za Bwana kwa Imani. Ewe mtu wa Mungu unatakiwa kujua majeshi ya Bwana hayatulii muda wote yanamlinda mteule. Je, wewe unamtegemea mtu wa namna gani? Wapo watu waliwategemea waume zao lakini waliawaacha na ikapaki “Ole”. Siku ya leo natakakusema na wewe kuwa mtegemee Mungu, kijana na wewe binti mtegemee Mungu. Watu wanaweza kushindwa lakini Jehova hawezi kushindwa kamwe. Mungu akubariki sana.

Ukitaka kufika kanisa la Mlima wa Moto Assembelies of God lipo Mikocheni “B” Dar es Salaam Tanzania, shuka Mwenge uliza madereva wa bodaboda au bajaji wakupeleke Mikocheni B kwa Mama Gertrude Rwakatare.

Tembele www.moountainoffire.blogspot.co au www.rumaafrica.blogspot.com

 




Comments